Marasimu hiyo ni sehemu ya mfululizo wa maombolezo yanayotarajiwa kuendelea kwa siku kadhaa katika maeneo mbalimbali ya Iran, ambapo waumini hujitokeza kumuenzi Bibi Fatimah (a.s) kwa ibada, matamko ya huzuni na ufafanuzi wa mafundisho yake.

23 Novemba 2025 - 22:46

Usiku wa Kwanza wa Maombolezo ya Kuadhimisha Shahada ya Bibi Fatimah (a.s), Kwa Uongozi wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatollah Khamenei +Picha

Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Katika Mji Mkuu wa Iran, Tehran, Waumini na wapenzi wa Ahlul Bayt (a.s) wamejitokeza kwa wingi kushiriki katika usiku wa kwanza wa maombolezo ya kuadhimisha shahada ya Bibi Fatimah Zahra (a.s) - binti wa Mtume Muhammad (s.a.w.w). Mkusanyiko huo umefanyika kwa hali ya unyenyekevu, huzuni na ibada, huku ukiongozwa na Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatollah Sayyid Ali Khamenei.

Ibada na maombolezo hayo yamejumuisha:

1_Hotuba za kiroho zinazobainisha nafasi tukufu ya Bibi Fatimah (a.s) katika Uislamu

2_Maatam na utenzi wa kumkumbuka Bibi Zahra (a.s)

3_Ibada za kusoma Qur’an na dua maalum

4_Wananchi kutoka tabaka mbalimbali walihudhuria ibada hizo na Marasimu hiyo ya Maombolezo ya Shahada ya Kipenzi cha Mtume wetu Muhammad (saww), Sayyidat Fatima Al-Zahra (sa).

Usiku wa Kwanza wa Maombolezo ya Kuadhimisha Shahada ya Bibi Fatimah (a.s), Kwa Uongozi wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatollah Khamenei +Picha

Katika hotuba, wazungumzaji wametoa msisitizo juu ya:

✓Uadilifu, ucha Mungu na ushujaa wa Bibi Fatimah (a.s)

✓Mchango wake katika kuhifadhi ujumbe wa Uimam na Mapinduzi ya Kiislamu

✓Umuhimu wa kuiga maisha yake katika jamii za Kiislamu.

Marasimu hiyo ni sehemu ya mfululizo wa maombolezo yanayotarajiwa kuendelea kwa siku kadhaa katika maeneo mbalimbali ya Iran, ambapo waumini hujitokeza kumuenzi Bibi Fatimah (a.s) kwa ibada, matamko ya huzuni na ufafanuzi wa mafundisho yake.

Usiku wa Kwanza wa Maombolezo ya Kuadhimisha Shahada ya Bibi Fatimah (a.s), Kwa Uongozi wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatollah Khamenei +Picha

Your Comment

You are replying to: .
captcha